RC IRINGA AZINDUA LISHE YA MIFUGO KUTOKA YARA TANZANIA
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MKUU
wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego ameisifu kampuni ya Utengenezaji na
Usambazaji wa mbolea nchini ya Yara Tanzania kwa kuzindua huduma mpya
nchini Tanzania ya Lishe ya Mifugo mbalimbali itakaowezesha wafugaji
kuwanenepesha Mifugo Yao na kuwa kwenye ubora unaotakiwa kitaifa na
kimataifa.
Alisema kuwa kampuni ya Yara ni
mdau mkubwa sana wa maendeleo ya sekta ya kilimo nchini na inafahamika
kwa ubora wa bidhaa zake, hususan mbolea mbalimbali za kupandia na
kukuzia mazao.
Aliongeza kuwa Ubora huo wa
bidhaa kutoka Yara, pamoja na maarifa wanayoyatoa kila wakati kwa
wakulima umeifanya kampuni hiyo kupendwa na kujikita katika mioyo ya
wadau wa hii sekta muhimu hivyo basi, ni furaha kuona kwamba Yara
Tanzania sasa imepanua wigo wake na kuongeza huduma mpya ya uzalishaji
na usambazaji wa lishe bora kwa mifugo
."Nawapongeza
sana Yara kwa uamuzi huu ambao sio tu muhimu kwa wafugaji kote nchini
bali pia kwa uchumi endelevu wa taifa letu.
Dendego alisema kuhusu Lishe Mpya ya Mifugo ni dhamira ya Yara ya kutaka kuleta mageuzi chanya na dhabiti ya sekta ya mifugo.
Alisema
kuwa Uzinduzi huu wa lishe mpya na bora ya mifugo ni ishara tosha
kwamba Yara wanatambua mchango wa wafugaji na wavuvi katika kuboresha
maisha ya watanzania na kuchangia ukuaji wa kipato cha mtu mmoja mmoja
na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Alisema
Serikali inatambua nafasi ya kipekee ya wafugaji katika kutekeleza
mikakati ya serikali ya kuinua uzalishaji wa maziwa, nyama na mayai humu
nchini.
Aidha alisema uzinduzi huu wa leo wa
lishe bora ya mifugo kutoka Yara utachangia kwa kiasi kikubwa kuchochea
uzalishaji wa bidhaa za ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku na hata
samaki.Licha ya kwamba Tanzania ni ya Tatu barani Afrika kwa wingi wa
mifugo, uzalishaji wetu wa maziwa, nyama na mayai bado ni wa kiwango
duni sana kutokana na sababu mbalimbali.
"Uchangiaji
wa sekta ya mifugo katika ukuaji wa uchumi wetu kwa kiwango cha 7% ya
pato la taifa pia ni wa chini mno. Hivyo basi juhudi za pamoja kati ya
sekta ya umma na binafsi zinahitajika kukuza uzalishaji na kuokoa kiasi
kikubwa cha fedha za kigeni" Alisema.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yara Tanzania, Winstone
Odhiambo alisema kwamba kampuni hiyo inayojihusisha na uagizaji na
usambazaji wa mbolea hapa nchini hadi sasa ni kampuni tanzu ya Yara
International ASA , ambayo inaongoza katika uzalishaji wa mbolea duniani
na katika masuala ya utunzaji wa mazingira na lishe.
Alisema
kampuni Ina Lengo la kuwawezesha wafugaji kupitia utoaji wa bidhaa mpya
za lishe bora ya wanyama mifugo ambazo zitabadilisha sekta ya mifugo na
uvuvi nchini na kuongeza kuwa bidhaa hizi za kulisha wanyama
zitakazopatikana kupitia mtandao wa wakala wasambazaji wa Yara Tanzania
nchini zitasaidia mamilioni ya wafugaji wa Wanyama kama vile ng’ombe,
mbuzi, kondoo, kuku na samaki ili kuongeza faida zao kulingana na
mabadiliko ya hali ya hewa.
"Yara
International inazalisha bidhaa za lishe bora za wanyama ambazo leo
tunazindua kwenye soko la Tanzania na Tunajisikia furaha na tutaendelea
kufanya kazi kwa karibu na serikali, wafugaji na wazalishaji wa chakula
cha mifugo ili kuboresha wingi na ubora wa uzalishaji wa maziwa, nyama,
mayai na Samaki" alisema
Odhiambo
alisema kuwa Bidhaa za Yara za lishe za mifugo zinatengenezwa kwa
viwango na ubora wa hali ya juu katika kiwanda cha kisasa cha Yara
nchini Afrika Kusini ambapo zitapatikana na kusambazwa nchini Tanzania
kwa bei ya ushindani.
"Uzinduzi wa leo hapa
Iringa ni muhimu kwa Tanzania, ukifuatia mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya
Chakula la Afrika (AGRF) uliofanyika hivi karibuni Dar es Salaam ili
kuhamasisha nchi za Afrika kuchukua hatua za kuhakikisha usalama wa
chakula, kumaliza umaskini na kulilitea bara hili mafanikio," alisema
Aliongeza
kuwa Tanzania ni nchi ya tatu barani Afrika kuanzisha lishe ya mifugo
kutoka Yara International baada ya Afrika Kusini na Kenya. Bidhaa hizi
zimekuwa zikitumiwa Ulaya kwa miongo kadhaa ambapo sekta ya mifugo
imekua kuwa biashara ya mabilioni ya dola.
Baadhi ya wafanyabiashara walisema huduma hiyo ni muhimu kwa ajili ya kuongeza ubora kwenye Mifugo ya wafugaji.
Mmoja
wa wafanyabiashara wa bidhaa za kilimo Mkoani Iringa, Mkurugenzi wa
Meja Agrovet Supply , Majorino Yangi alisema kuwa huduma hiyo hiyo
imekuja kwenye wakati mwafaka na kuwaponyeza Yara kwa kuzindua rasmi
Lishe ya Mifugo ambayo itasaidia wafugaji kukuza Mifugo Yao katika njia
nyingine tofauti na awali.
No comments