LHRC chawakutanisha Wadau Kutathimini Miaka 30 ya Demokrasia Tanzania
Wadau mbalimbali wakishiriki katika Mjadala katika Maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
KATIKA
kuadhimisha Siku ya Demokrasia Duniani, Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC) kimewakutanisha wadau kutathmini Miaka 30 ya Demokrasia
tangu kuanzishwa kwa Vyama Vingi vya Siasa nchini mwaka 1992.
Akizungumza
katika mjadala huo uliofanyika jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa
LHRC Felista Mauya amesema kuwa LHRC ni mdau na mtetezi mkubwa wa haki
za binadamu.
“Kuadhimisha siku hii ni kuendeleza jitihada za kukuza na kulinda haki za binadamu,” amesema Felista.
Felista
ameeleza kwamba Demokrasia ni kielelezo tosha cha ustawi wa haki za
binadamu, pia ni ishara ya kuendeleza utamaduni wa ustaarabu na utii wa
Sheria. Kwamba uwepo wa Demokrasia ni kiashiria cha utekelezaji wa dhana
ya ushiriki na ushirikishwaji wa wananchi katika kufanya maamuzi ya
kuchaguaviongozi wao.
Dkt.
Bujari ameendeelea kueleza kuwa ili kufikia malengo ya kutokomeza
maradhi ya Kifua Kikuu na UKIMWI, kwa miaka mitatu ijayo, zinahitajika
Dola za kimarekani bilioni 130.2 na Global Fund pekee yake inahitaji
dola za kimarekani bilioni 18.
Kwamba
fedha hizo zitachangia kuendeleza mapambano ya kutokomeza maradhi hayo
kwa kujenga ustahamilivu na mifumo ya endelevu ya afya na kuimarisha
utayari katika kukabiliana na maradhi, hasa katika nchi zinazoendelea
kama Tanzania ambapo hiyo itasaidia kufikia watu milioni 20 ifikapo
mwaka 2026.
Amesema
katika Sekta ya Afya kwa Tanzania pekee, mfuko huo umeweza kuchangia
kiasi cha Dola za kimarekani bilioni 2.6 toka mwaka 2002 ambapo fedha
hizo zimesaidia kupambana na magonjwa ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria.
Kwamba
zaidi ya watu milioni 1.2 waliweza kufikiwa na kupata huduma za dawa za
kufubaza makali ya virusi vya ukimwi, zaidi ya watu milioni 8.2
wamepata huduma na kupona Malaria, neti milioni 4 zimegawiwa bure nchi
nzima, zaidi ya watu elfu 84 wamepona Kifua Kikuu na zaidi ya watu 391
wenye Kifua Kikuu sugu wapo kwenye matibabu.
“Kiwango cha VVU hapa Tanzania pia kimeshuka kutoka xxx mwaka mpaka xx mwaka 2016,” amesema Dkt. Bujari.
Amebeinisha
kuwa kidunia Mkutano Mkuu wa uchangiaji wa Mfuko kwa Awamu ya saba
utafanyika nchini Marekani kuanzia Septemba 19 hadi 21 mwaka huu kwamba
fedha hizo zinategemewa kuokoa maisha ya wanadamu zaidi ya milioni 20
duniani kote ifikapo mwaka 2026.
WADAU WAZUNGUMZIA HALI YA DEMOKRASIA NCHINI
Mwenyekiti
wa Chama Cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba akichangia katika
mjadala, amesema kwamba hali ya Demokrasia nchini imekuwa ikisuasua
katika kipindi cha miaka sita iliyopita.
“Tume
ya Jaji Nyalali ilipendekeza kuandika Katiba Mpya na kufanya mabadiliko
ya Sheria 40. Kuliendelea mbele bila kuwa na msingi mzuri wa kikatiba
na sheria,” ameeleza Prof. Lipumba.
Mbunge wa Ubungo (CCM) Profesa Kitila Mkumbo amesema, ili wananchi washiriki vizuri katika Demokrasia ni lazima miiba iondolewe.
“Ni
vizuri iandikwe Katiba ambayo itaongeza ushiriki wa wananchi katika
Demokrasia. Katiba ikiendelea namna hii, mtaendelea kulia kila mwaka,”
amesema Prof. Mkumbo.
Naibu
Katibu Mkuu Bara wa ACT-Wazalendo Joram Bashange amesema “Tunahitaji
kuwekeza kwa wananchi kwenye elimu ya Uraia,”. Ameeleza kuwa kama
ACT-Wazalendo wametoa mapendekezo yao kwenye kikosi kazi kwamba
ubadilishwe mfumo wa uchaguzi.
“Tutoke
kwenye first past the post, twende kwenye proportional representation.
Hii itaongeza ushiriki wa wananchi katika Demokrasia,” amesema.
Kwa
upande wake Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Neema Rugangira amesema kuwa ni
vizuri kukawa na utaratibu wa kutenga nafasi Fulani za majimbo kwa
ajili ya wanawake kwamba hiyo itavifanya vyama kuwajengea uwezo
wanawake.
Post Comment
No comments