Breaking News

MOI, Hospitali Ramaiyah zaweka kambi kufanya Upasuaji Uvimbe kwenye Ubongo, Uti wa Mgongo


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

TAASISI ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Ramaiah ya nchini India imewafanyia upasuaji wagonjwa 12 wenye uvimbe kwenye ubongo na matatizo kwenye uti wa mgongo.

Kwa mujibu wa MOI ni kwamba kila siku
imekuwa inapokea wagonjwa watatu wenye tatizo la kiharusi 'stroke' na kwamba tatizo hilo limekuwepo kwa muda mrefu na wanaendelea kutafuta Teknolojia zaidi ya kuutibu ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo Laurent Mchome alipokuwa akizungumza na wanahabari mbalimbali waliokuwa katika kambi maalumu ya upasuaji wagonjwa 12 wenye matatizo ya uvimbe kwenye ubongo na matatizo yanayohusu utu wa mgongo.

Amebainisha kuwa kwenye kambi hiyo ya siku tatu inafanyika kwa ushirikiano kati ya taasisi ya MOI pamoja na Hospitali ya Ramaiyah Medical Collage Memorial ya Bangalore ya India huku akifafanua tatizo la kiharusi limekuwepo kwa muda mrefu na wanaendelea kutafuta teknolojia zaidi ya kuutibu ugonjwa huo.

Amesisitiza kuwa kuna aina nyingi za kiharusi lakini wagonjwa wengi unapwapata ni wale ambao damu imevilia kwenye ubongo,tatizo hilo ni kubwa sana na kwenye maabara yao wanawafanyia uchunguzina wakiona wanahitaji upasuaji ndipo wanawafanyia upasuaji.

Ameongeza kuwa miaka ya nyuma wagonjwa hao walikuwa wakipatiwa huduma saidizi na wakipata nafuu hupelekwa nje ya nchi kutibiwa akini sasa wanatibiwa hapa nchini."Chanzo kikubwa cha tatizo hilo ni shinikizo la juu la damu.

Dk.Mchome amesema kuna wagonjwa wengi ambao Wanashinikizo la juu la damu ambao hawatumii dawa kwa kufuata mpangilio maalumu walioelekezwa na wataalamu, hivyo wapo kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo.

"Kuna wengine ambao wanaopata lehemu kwenye damu na wao wapo kwenye hatari ya kupata vivimbe ambavyo hupasuka na mtu kupata kiharusi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respecius Borniface amezungumzia kuhusu kambi maalumu ambayo imeanza Septemba 19 na itaendelea hadi Septemba 21.Katika kambi hiyo wanatarajia wagonjwa 12 watafanyiwa upasuaji mkubwa wa kibobezi.

Amefafanua kuwa kati ya hao wagonjwa saba watafanyiwa uchunguzi wa tiba kichwani bila kufungua fuvu, watano ambapo kati ya hao 12 wapo watakaofanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo kupitia tundu dogo.



No comments